Uwezo wa kuelekeza kwa uwazi na kurahisisha mada ngumu ili kueleweka kwa wote.
Uwezo wa kurekebisha kasi na mbinu za ufundishaji kulingana na uwezo na mahitaji ya kila mwanafunzi.
Uwezo wa kujenga mazingira rafiki ya ujifunzaji kwa kushirikiana, kutoa ushauri na kujenga mshikamano na mjifunzaji.
Uwezo wa kupima maendeleo ya mjifunzaji mara kwa mara na kutumia mrejesho kuboresha ufundishaji.
40+
10,389
34,177
793,361
Kuwa mwezeshaji katika jukwaa hili kunakuwezesha kukuza ujuzi wa kitaaluma na uongozi, kupata uzoefu wa vitendo wa ushauri na ufundishaji, kupanua mtandao wa kitaaluma, na kujijengea sifa na mchango chanya katika maendeleo ya elimu ya jamii. Pia hukupa nafasi ya kujifunza kutokana na mitazamo na uzoefu wa wengine, jambo linalokuza uelewa mpana wa taaluma yako. Aidha, ushiriki huu huongeza uwezo wako wa mawasiliano, ujasiri wa kitaaluma, na kuongeza thamani yako.
Lengo la kozi hii ni kuwajengea washiriki maarifa, ujuzi, na mielekeo inayohitajika ili kuwezesha ujifunzaji bora kupitia uelekezaji mzuri, ushirikiano na utatuzi wa changamoto za kila mjifunzaji.
Unatarajiwa kudhihirisha uwezo wa kuwaunga mkono wajifunzaji, kuwasiliana kwa uwazi, kutoa mrejesho wenye tija, na kuchangia mabadiliko kwa mjifunzaji kupitia uratibu na uwezeshaji (mentorship).
Ili kuwa mwezeshaji katika jukwaa hili, unahitaji kujaza fomu ya maombi, kuwasilisha sifa zako za kitaaluma, na kuonesha uzoefu au nia ya kusaidia wengine kujifunza. Baada ya hapo, maombi yako yatapitiwa, na ukikidhi vigezo, utaidhinishwa na kuanza kushiriki katika shughuli za uwezeshaji, ushauri, na ufuatiliaji wa maendeleo ya wanafunzi.
Je, ungependa kuungana nasi katika safari ya kuhudumia jamii?
Fahamu zaidi... WhatsAppUtaziwezesha kozi zako kwa kuandaa na kupakia muhtasari na maudhui ya kozi, kusambaza na kufundisha wajifunzaji watakaopatikana, kutoa kazi za upimaji na kutoa mrejesho wa mara kwa mara kwa washiriki. Jukwaa linakuruhusu kutumia zana za kidijitali kama video, nyaraka, majadiliano kupitia sehemu ya ujumbe pamoja na njia nyingine HALALI ili kuhakikisha ujifunzaji shirikishi, unaoeleweka, na unaolenga matokeo bora.
Je, ungependa kufahamu zaidi?
Mwongozo Sera & FaraghaUtawapata wajifunzaji kwa kutangaza kozi zako kupitia jukwaa hili pamoja na majukwaa mengine unayoweza kuyafikia, pamoja na kuwasilisha maudhui yenye kiwango kinachoendana na mahitaji ya wadau, na kujenga wasifu kuaminika. Kuwadumisha hao wajifunzaji inategemea ufundishaji shirikishi, mawasiliano ya mara kwa mara, mrejesho wenye kujenga, kujitoa katika kutatua changamoto zao za ujifunzaji na kuweka mazingira rafiki yanayochochea ushiriki na mwendelezo wa ujifunzaji.
Lengo la kozi hii ni kuwajengea washiriki maarifa, ujuzi, na mielekeo inayohitajika ili kuwezesha ujifunzaji bora kupitia uelekezaji mzuri, ushirikiano na utatuzi wa changamoto za kila mjifunzaji.
Unatarajiwa kudhihirisha uwezo wa kuwaunga mkono wajifunzaji, kuwasiliana kwa uwazi, kutoa mrejesho wenye tija, na kuchangia mabadiliko kwa mjifunzaji kupitia uratibu na uwezeshaji (mentorship).
Malipo ya kozi zako yatafanyika kwa mujibu wa taratibu na masharti ya jukwaa hili. Baada ya wanafunzi kujiandikisha na kukamilisha malipo, gawio lako litawekwa kwenye akaunti yako ya Mwezeshaji. Malipo yatahamishwa kwako kupitia njia rasmi za malipo zilizothibitishwa, kama vile huduma za fedha kwa simu au akaunti ya benki, kulingana na chaguo ulilochagua. Taarifa zote za malipo zitapatikana kwenye Dashibodi yako kwa uwazi na ufuatiliaji rahisi.
Je, ungependa kufahamu zaidi?
Vigezo & Masharti Sera & Faragha